UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna mpango wa kutwaa Kombe la Ligi Kuu Bara kutokana na kuachwa kwa pointi nyingi na mpinzani wao Simba ambaye anaongoza Ligi Kuu Bara kwa sasa.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 51 ikiwa imecheza mechi 27.
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa kwa sasa ni lazima aseme ukweli kwamba kikosi chake hakina uwezo wa kutwaa Kombe la Ligi Kuu Bara kutokana na kuachwa pointi nyingi na Simba.
“Ukiwa kocha wakati mwingine unakuwa kwenye hali ambayo hakuna anayeweza kukuelewa kile ambacho utasema kwa mfano muda huu nikisema sina uwezo wa kutwaa kombe wengi wanaweza wakadhani nimekata tamaa hapana.
“Muda mwingine ni lazima niseme ukweli ukitazama mahali nilipo na wapinzani wangu walipo ni mbali hivyo kazi yangu kubwa ni kuwajenga kisaikolojia wachezaji ili wakati ujao sasa wawe na nguvu ya kulisaka kombe ila kwa sasa tusubiri na tuone itakuaje,” amesema.
Yanga imezidiwa kwa jumla ya pointi 20 na Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ambayo imesimama kwa muda wa mwezi mmoja ili kupisha maambukizi ya virusi vya Corona.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.