SOLLY Njashi Mwenyekiti wa Mbao FC ya Mwanza amesema kuwa wameamua kuiuza timu hiyo kwa mtu yeyote ambaye atakuwa tayari kuinunua aendelee kuiendesha.
Njashi amesema kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na timu kujiendesha katika mazingira magumu kutokana na kukosa fedha za kuiendesha timu hiyo.
“Sababu za kuuza timu ni kutokana na uendeshaji wake kuwa mgumu kwani tumekuwa tukiendesha timu katika mazingira magumu na wachezaji wengi hawajalipwa mshahara jambo linalowafanya wacheze wakiwa hawana morali kubwa,” amesema.
Mbao inashiriki Ligi Kuu Bara kwenye msimamo ipo nafasi ya 19 imecheza mechi 29 kibindoni ina pointi 23.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.