VIONGOZI watano ndani ya Klabu ya Yanga kwa sasa wameenguliwa kwenye uongozi ndani ya Klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani kutokana na sababu mbalimbali.
Kati ya viongozi hao wawili wameenguliwa na Kamati ya Utendaji ya Yanga kutokana na masuala ya kinidhamu huku watatu wakikubaliwa kujiuzuru nafasi zao ndani ya Yanga.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dk Mshindo Msolla imeeleza kuwa :-Kamati ya Utendaji ya Yanga imechukua hatua ya kinidhamu ya kuwasimamisha wajumbe wawili wa kamati hiyo ambao ni Salim Rupia na Frank Kamugisha Machi 27 mpaka mkutano Mkuu itakapofanya maamuzi kwa mujibu wa Katiba ya Yanga.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha siku mbili kilifanyika Machi 26 na Machi 27 baada ya kutokea sintofahamu na kupelekea mdhamini wa Klabu ya Yanga, Kampuni ya GSM kujitoa udhamini wa masuala yasiyo ya kimkataba.
Pia kamati imepokea na kukubali maombi ya wajumbe watatu ambao ni Rogers Gumbo, Shija Richard na Said Kambi
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.