MABEKI wawili ndani ya Simba inaelezwa kuwa nafasi yao ya kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2020/21 ni ndogo kutokana na kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza hivyo panga linawahusu.
Nyota hao ni Paul Bukaba anayekipinga ndani ya Namungo kwa mkopo inaelezwa hajaweza kureea kwenye ubora wake pamoja na Yusuph Mlipili ambaye yupo Simba kwa sasa.
Mlipili, Simba ikiwa imecheza mechi 28 za Ligi Kuu Bara hajapata nafasi ya kuanza kwenye mechi hizo huku Bukaba akizidi kujiimarisha ndani ya Namungo.
Habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa ni kwamba Simba inataka kuboresha kikosi chake kwa kuleta nyota wengine ambao watachukua nafasi za wachezaji hao.
“Ili Simba ilete wachezaji ni lazima wengine waondoke kwani wapo wengi na nafasi zao pia zimekuwa finyu hivyo ni wakati wa kuangalia namna gani panga litawapitia,” ilieleza taarifa hiyo.
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck hivi karibuni alisema kuwa kwa wachezaji alionao kwenye kikosi chake wale ambao hawaanzi kikosi cha kwanza ni kutokana na juhudi wanazoonyesha kwenye mazoezi.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 kwenye msimamo.