Uncategorized

DITRAM NCHIMBI: NINACHUKUA TAHADHARI YA CORONA NA KULINDA KIPAJI

admin March 31, 2020 9:21 pm


DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa sasa anaendelea na programu aliyopewa na Kocha Mkuu Luc Eymael ili kulinda kipaji chake.

Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa janga la dunia kwa sasa.

Mshambuliaji huyo anayeaminika kutumia nguvu nyingi uwanjani kuwasumbua mabeki yupo zake mkoani Songea baada ya ligi kusimama.

Nchimbi mwenye mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara na pasi mbili za mabao amesema kuwa anatambua umuhimu wa kuchukua tahadhari kwa ajili ya kujilinda na Virusi vya Corona pamoja na kuendelea kufuata programu alizopewa na kocha ili kulinda kipaji chake.

 “Nipo vizuri ninaendelea na mazoezi ambayo nimepewa programu na kocha hilo ni muhimu kwani kazi yangu ni mchezaji na ninaendelea na mazoezi,” amesema.

HAWA HAPA WANAHUSIKA KWENYE MABAO YA MUUAJI WA SIMBA KIUNGO MPYA WA AZAM FC APEWA PROGRAMU YAKE ILI KUFANYA MAKUBWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply