Home Uncategorized JISHINDIE GARI, BABA LAO HIVI NDIVYO ILIVYOTINGA KAWE

JISHINDIE GARI, BABA LAO HIVI NDIVYO ILIVYOTINGA KAWE


WASOMAJI mbalimbali wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra wa maeneo ya Kawe, Mikocheni hadi Msasani mapema jan walijaza kuponi kwa ajili ya kushiriki droo ya Bahati nasibu ya Shinda gari  iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya  inapatikana kupitia magazeti hayo yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers.
Timu ya maofisa masoko wa Publishers walitembelea maeneo hayo na kushuhudia wasomaji wakijaza kuponi kwa ajili ya kuingia katika droo ya bahati nasibu hiyo ambayo mshindi atanyakua ndinga mpya aina ya FunCargo.
Akipiga stori na wasomaji hao Ofisa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam,  amewasisitiza wananchi hao kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili waweze kuwa miongoni mwa washindi wataoinyakua ndinga hiyo.
‘Niwasihi wakazi wa Kawe na maeneo mengine muendelee kununua magazeti yetu ili muwe miongoni mwa washindi, tutatoa gari mpya siku ya mwisho ya droo na kabla ya droo kubwa wapo ambao kila wiki watakuwa wanajinyakulia simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.
JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie GariGlobal PublishersS.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.
MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here