Uncategorized

SAINI YA JADON SANCHO DILI KUBWA KWA TIMU KUBWA, CHELSEA NA UNITED ZAMUWANIA

admin March 29, 2020 6:21 am

KLABU ya Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu Frank Lampard imevutiwa na uwezo wa nyota anayekipiga ndani ya Borrusia Dortmund, Jadon Sancho.
Hesabu za Lampard zinagogana na Kocha Mkuu wa Manchester United Ole Gunnars Solskajer ambaye naye pia anapendezwa na uwezo wa nyota huyo Sancho.
Timu zote kwa sasa mpango wao ni kuona namna gani zitapata saini ya Sancho lakini inaelezwa kuwa dau linaweza kuwa tatizo kwa sasa kutokana na klabu nyingi kupitia kwenye wakati mgumu kiuchumi kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona. 
Sancho amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ndani ya Bundesliga timu yake ikiwa imecheza mechi 23 ametupia mabao 14 na kutoa pasi 15 za mabao.

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU KUJIUZULU KWA VIONGOZI WAO PAMOJA NA WALE WALIOJIENGUA HIVI NDIVYO NYOTA WA POLISI TANZANIA ANAVYOLINDA KIPAJI CHAKE WAKATI HUU WA MAPUMZIKO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply