Home news KUHUSU USAJILI MPYA MSIMBAZI..SENZO EMEFUNGUKA HAYA..!!

KUHUSU USAJILI MPYA MSIMBAZI..SENZO EMEFUNGUKA HAYA..!!

WAKATI baadhi ya majina ya wachezaji wakihusishwa na Simba, uongozi wa klabu hiyo umesema tayari umepokea mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mbelgiji Sven Vandenbroeck na kuanza kuyafanyia kazi kimya kimya.

Akizungumza na gazeti la Nipashe jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, alisema kwa sasa wanafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi kwa wachezaji ambao wataongezwa pamoja na watakaochwa kutokana na matakwa ya ripoti ya kocha huyo.

Msauzi huyo alisema mikakati yao mikubwa ni kufanya usajili kwa ajili ya kuandaa kikosi cha timu hiyo kuweza kutoa ushindani mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa ikiwamo kuvuka katika hatua ambayo waliishia msimu uliopita.

“Kwa sasa Sven ametoa mapendekezo yake ya wachezaji wa kusajiliwa na kuachwa, hili linafanyiwa kazi kwa umakini, hatuwezi kuweka wazi siri za klabu muda ukifika kila kitu kitajulikana,” alisema Senzo.

Wachezaji ambao Simba inadaiwa kuanza kufanya nao mazungumzo ni beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto kwa kuchukua kiasi cha Sh. milioni 80 licha ya nyota huyo kudai thamani yake ni Sh. milioni 90.

Wengine waonatajwa ni Mghana James Kotei anayecheza soka la kulipwa Belarus, Emmanuel Okwi anayekipiga Al Ittihad ya Misri, pia kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ambaye jina linadaiwa linajadiliwa na kamati ya usajili ya vinara hao wa Ligi Kuu Bara

SOMA NA HII  BALAA LA LEO UWANJANI LILIKUWA NAMNA HII, MATOKEO HAYA HAPA