KLABU ya Alliance School yenye maskani yake mkoani Mwanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara imeweka rekodi ya kuwachimbisha makocha wanne kazi mazima.
Ikiwa kwa sasa msimu wa 2019/20 umesimamishwa na Serikali kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona tayari makocha wanne wamepigwa chini ndani ya Alliance.
Kocha wa kwanza kutimuliwa msimu huu ndani ya ligi alikuwa Athuman Bilali wengi hupenda kumuita Bilo alisimamia mechi moja ya ufunguzi dhidi ya Mbao FC na dakika tisini zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Wengine ambao maisha yao yalikuwa mafupi ni pamoja na Habib Kondo, Malale Hamsin ambaye kwa sasa anainoa Polisi Tanzania pamoja na Fred Felix Minziro ambaye bado yupo ndani ya Alliance ila sio kwenye benchi la ufundi.
Alliance ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo kibindoni ina pointi 29 baada ya kucheza mechi 29. Bilo baada ya kuchimbishwa alisema kuwa alikuwa anapangiwa kikosi pamoja na kutopewa ushirikiano na benchi la ufundi jambo lililomponza.
Makamu Mwenyekiti wa Alliance, Stephano Nyaitati amesema kuwa uongozi unafuata misingi ya kazi na hauna tabia ya kuingilia majukumu ya makocha.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.