Home Uncategorized BABY J AJA NA MKWARA MZITO KWA ATAKAYEMROGA

BABY J AJA NA MKWARA MZITO KWA ATAKAYEMROGA


MWANAMUZIKI maarufu wa visiwani Zanzibar, Jamila Abdallah ‘Baby J’ amesema kuwa zamani watu wengi walikuwa wakipenda kucheza na mwili wake lakini sasa hivi yuko imara sana hakuna wa kumchezea na atakayejaribu, anatafuta kifo.

Akizungumza na Amani, Baby J alisema zamani walitaka kabisa kumfanya kichaa na ndiyo maana akawa asikiki kabisa kwenye muziki, lakini kwa sasa anamshukuru sana Mungu amepona na yuko vizuri.

“Yaani sasa hivi mtu yeyote anayejiweza anisogelee aone balaa lake, maana najua anatafuta kifo kibaya kwa sababu nimejilinda vilivyo,” alisema Baby J.
SOMA NA HII  LIGI KUU BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI, ISHU YA VIPORO YAPATA DAWA