Uncategorized

ANAYEWINDWA NA YANGA AANZA KUAGA RASMI KWA MABOSI WAKE

admin April 17, 2020 8:01 am


PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli ambaye saini yake inaelezwa inawindwa na mabosi wake wa zamani Yanga amewaaga mabosi wake wa Lipuli rasmi ili asepe msimu ujao.

Nonga amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya Lipuli akiwa amefunga mabao 11 na kutoa pasi nne za mabao kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mkataba wake ndani ya Lipuli umebakisha miezi sita ambapo tayari mabosi hao walianza kufanya naye mazungumzo ili kupata saini yake msimu ujao.

“Nimewaambia viongozi wa Lipuli kwamba kwa sasa ninahitaji kupata changamoto mpya ili waaanze kutafuta mbadala wangu mapema kwani msimu ujao ninaondoka,” amesema Nonga.

Chanzo: Championi

KUMEKUCHA, KIUNGO MWINGINE NDANI YA SIMBA APIGIWA HESABU NA TP MAZEMBE IBRAHIM AJIBU ANAFANYA HIVI KULINDA KIPAJI CHAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply