Uncategorized

IBRAHIM AJIBU ANAFANYA HIVI KULINDA KIPAJI CHAKE

admin April 17, 2020 8:31 am


IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji ndani ya Simba amesema kuwa wakati huu wa mapumziko ya Ligi Kuu Bara kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona amekuwa akichukua tahadhari huku akifanya mazoezi kulinda kipaji chake na kujitoa kwa jamii.

Ajibu amesema kuwa amekuwa akitoa misaada kwa jamii ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Nimekuwa nikifanya mazoezi ili kulinda kipaji changu kwani kwa sasa ligi imesimama na hakuna ambacho kinaendelea zaidi ya mazoezi binafsi ambayo kila mmoja anapaswa kufanya.

“Pia nimekuwa nikitoa misaada kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na Virusi vya Corona nami nimekuwa nikichukua tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima,” amesema.

ANAYEWINDWA NA YANGA AANZA KUAGA RASMI KWA MABOSI WAKE HATMA YA NYOTA WA ZAMANI WA YANGA IPO KWA MROMANIA WA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply