Uncategorized

KOCHA YANGA ATAJA KINACHOWAPONZA MAKIPA BONGO KUPOTEZWA NA WAGENI

admin April 18, 2020 9:31 am

PETER Manyika, Kocha wa makipa ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa viwango vya magolikipa wa kigeni ni vya kawaida ukilinganisha na vile vya wazawa kutokana na kile wanachokionesha wawapo uwanjani ila ni wavivu.

Manyika amesema kuwa wengi wamekuwa wakifanya sawa na wazawa jambo ambalo anaamini wanatoshana nguvu.

“Wachezaji wakigeni bado uwezo wao ndani ya ligi ni wa kawaida sawa na wazawa ila tofauti yao ni ndogo tu kujituma.

“Kinachowashinda wazawa wengi ni uvivu wa kutopenda kufanya mazoezi na kujituma zaidi uwanjani ila wakiamua wanaweza kuwa bora zaidi,” amesema.

Miongoni mwa makipa ambao ni wageni na wanafanya vizuri ndani ya Bongo ni pamoja na Nurdin Barola anayekipiga ndani ya Namungo FC.

Pia kwa Azam FC yupo Razack Abarola ambaye ni kipa nammba moja.

MORRISON BALAA LAKE LILIKUWA NAMNA HII NDANI YA LIGI KUU BARA KIUNGO ALIYEKIPIGA SIMBA NA YANGA AMPA SOMO MWAMNYETO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply