Home Uncategorized JEURI YA PESA..!! SIMBA YAZUIA NYOTA WAKE 10 KUSEPA

JEURI YA PESA..!! SIMBA YAZUIA NYOTA WAKE 10 KUSEPA

JEURI ya fedha iliyoonyeshwa na Simba katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo imewatia pingu kwa muda wa misimu mitatu mfululizo nyota 10 wazawa tofauti wa klabu hiyo tofauti na awali.

Nyota hao ni wale waliokuwemo katika kikosi cha Simba tangu bilionea Mohamed Dewji aanze kutoa sapoti ya moja kwa moja ya kifedha na kisha baadaye kuwa mwekezaji wa asilimia 49. Mo ameonyesha jeuri kwa kuwabakisha wachezaji hao kila wanapotakiwa na timu nyingine ikiwemo Yanga na Azam kwa kuwaongezea dau kwa lengo la kuimarisha timu.

Ingawa zaidi ya wachezaji 15 wamepigwa panga na wengine kuipa mkono wa kwaheri Simba, uwepo wa nyota hao 10 hapana shaka umechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya timu hiyo kuwa tishio uwanjani kutokana na muunganiko mzuri walionao kwa kukaa pamoja kwa muda mrefu.

Wachezaji hao 10 ni kipa Aishi Manula, mabeki Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe na Yusuph Mlipili wakati viungo ni Jonas Mkude, Said Ndemla na Mzamiru Yassin na mshambuliaji ni John Bocco

Kipa Aishi Manula ambaye alisajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC ameendelea kuwa chaguo la kwanza katika nafasi ya kulinda lango na amekuwa muhimili imara katika lango la Simba kutokana na uwezo wake wa kuondosha hatari kutoka kwa washambuliaji wa timu pinzani.

Kudhihirisha mchango wa Manula ndani ya Simba, katika misimu yake miwili iliyopita ndani ya klabu hiyo ameweza kutwaa tuzo ya Kipa Bora mara mbili na upo uwezekano akatwaa tena msimu huu kwani hadi sasa amedaka mechi 15 (clean sheet) za Ligi Kuu bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa.

SOMA NA HII  MORRISON: JUMA ABDUL ASINGENIACHIA, NISINGEIFUNGA SIMBA