Uncategorized

THAMANI YA NYOTA WA PSG SOKONI YASHUKA GHAFLA

admin April 19, 2020 11:29 am


THAMANI ya mshambuliaji anayekipiga ndani ya Klabu ya PSG, Kylian ambappe imeripotiwa kuporomoka kwa kasi kwenye soko la wachezaji kutokana na janga la maambukizi ya Virusi vya Corona.

Awali thamani ya nyota huyo raia wa Ufaransa sokoni ilikuwa ni pauni milioni 189 na inatajwa inaweza kushuka zaidi ya hapo kufikia pauni milioni 150.

Cohn Bendit ambaye ni mbunge nchini Ufaransa na mwanachama wa Bunge la Umoja wa Ulaya anaamini kuwa thamani ya Mbappe itashuka zaidi kutokana na mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na maambukizi ya Virusi vya Corona ambao anaamini utaathiri pia sekta ya michezo.

Ripoti zinaonyesha kuwa ada za masuala ya usajili kwa wachezaji wengi zimeanza kuporomoka kwa kasi ghafla kutokana na timu nyingi kubana matumizi katika kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona.

HAWA HAPA LICHA YA KUPEWA KITAMBAA CHA UNAHODHA WANACHEKA NA NYAVU PIA KOCHA MKUU WA SIMBA AUKUBALI MUZIKI WA KIUNGO HUYU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply