Uncategorized

NAHODHA YANGA APANIA KUWA BORA ZAIDI MAISHA YAKIREJEA KAMA ZAMANI

admin April 21, 2020 2:29 pm


PAPY Tshishimbi, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa anaendelea kufanya mazoezi ili kulinda kipaji chake pamoja na kuchukau tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wapo nyumbani wakiendelea kufanya mazoezi binafsi.

Tshishimbi ambaye ni nahodha amesema:”Naendelea kujiimarisha kipindi hiki cha Corona lengo langu ni kuona kwamba  tukirejea kwenye maisha ya kawaida niwe kwenye kiwango changu ama zaidi katika kuitumika Yanga,” .

Yanga ikiwa imecheza mechi 27, Tshishimbi amecheza mechi 23 na ametoa pasi moja ya bao kwenye mechi dhidi ya Biashara United.

TEGETE AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI NI NYONI NA YONDANI TU..ISHU NZIMA IPO HIVI..!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply