Uncategorized

MESSI AJIFUNGIA NDANI KISA CORONA

admin April 22, 2020 8:35 am

RAMADHAN Singano,’Messi’ nyota kutoka Bongo anayekipiga ndani ya TP Mazembe ya nchini Congo amesema kuwa kwa sasa anashinda ndani akifanya mazoezi mepesi kutokana na zuio la Serikali kutowaruhusu kutoka nje.
Virusi vya Corona vimekuwa ni janga la dunia baada ya kuripotiwa kuanza kusambaa ambapo  kesi ya kwanza iligundulika nchini China, Desemba 2019.
Messi amesema kuwa kutokana na janga la Corona kwa sasa wanaendelea kufanyia mazoezi nyumbani baada ya zuio la Serikali.
“Kwa sasa tupo tunaendelea salama ila kwa upande wa mazoezi tunapigia nyumbani kwani hakuna ruhusa ya kuwa nje kutokana na kujikinga na Virusi vya Corona, ni maombi yetu hali iwe salama turudi kwenye wakati wetu kama zamani,” amesema Messi.
SIMBA YAKUBALI UWEZO WA KIUNGO WA YANGA ALIYEWAVURUGA MACHI 8 UWANJA WA TAIFA KOCHA KAGERA SUGAR AWATAKA WACHEZAJI WASIPUUZIE MAZOEZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply