Uncategorized

SARRI APEWA ZIGO LA LAWAMA NA KIUNGO HUYU ANAYEKIPIGA BORUSSIA DORTMUND

admin April 23, 2020 2:35 pm

KIUNGO wa Borussia Dortmund, Emre Can amefunguka kuwa aliyewahi kuwa kocha wake Maurizio Sarri alishindwa kumpa nafasi, lakini kwa kiasi alipata uzoefu.
Can amejiunga na Dortmund katika usajili wa dirisha dogo wa Januari akitokea Juventus ambako alikuwa hana nafasi kwenye kikosi cha Sarri.
Kiungo huyo  kilichomkimbiza zaidi Juventus ni kile kitendo cha kuachwa katika kikosi cha wachezaji ambao walikuwa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Can alisema: “Sarri  hakutaka kunipa nafasi ndani ya Juventus, nimepitia nyakati ngumu sana nikiwa pale na kocha yule.
“Nilikuwa mchezaji muhimu na bora mwaka mmoja kabla na baada ya kutwaa tajin kwa kucheza vizuri  michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Lakini pamoja na yote, Juventus kwangu inabaki kuwa sehemu nzuri na yenye kumbukumbu nzuri katika kazi yangu,”alisema Can.
 Kiungo huyo alijiunga na Juventus akiwa mchezaji huru kutoka Liverpool mwaka 2018 na akiwa hapo alicheza mechi 45 kufunga mabao manne na kutoa asisti moja.
NI MUDA WA KLABU ZOTE BONGO KUUNGANA KWENYE VITA HII, ILE VITA YA AWALI MUDA WAKE UMEISHA KWA WALICHOKIFANYA IHEFU WANASTAHILI KUWA DARASA, ILA HILI LA CORONA LISIPUUZWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply