Home Uncategorized KOCHA ATAJA KINACHOWAPONZA WACHEZAJI WA BONGO KUSHINDWA KUTUSUA

KOCHA ATAJA KINACHOWAPONZA WACHEZAJI WA BONGO KUSHINDWA KUTUSUA

PATRICK Mwangata, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Mtibwa Sugar amewaasa wachezaji nchini kumuiga nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika suala la nidhamu na uvumilivu pale wanapopata nafasi ya kwenda kujaribu maisha ya soka nje ya nchi.
Mwangata amesema kuwa wachezaji wengi wa Bongo hawana uvumilivu na nidhamu ya soka na ndiyo maana wengi wao hufanya majaribio nje ya nchi na kushindwa.
“Wachezaji wengi wa Kitanzania siyo wavumilivu huku pia suala la nidhamu kwa baadhi yao likiwa ni changamoto kubwa na hii ndiyo sababu wengi wanapata nafasi ya kwenda  nje kufanya majaribio lakini hurudi na visingizio vingi kama vile masuala ya masilahi au hali ya hewa kitu ambacho si sahihi.

 “Kama hilo lingekuwa tatizo basi Samatta asingefika alipo, lakini yeye alitanguliza nidhamu na uvumilivu mwisho ametutoa kimasomaso, hivyo ni muhimu nyota wetu wakajifunza kutoka kwake na kutambua kuwa ili kufi ka mbali unahitaji nidhamu ya kutosha na uvumilivu.
“Taifa letu linahitaji nyota wengi zaidi ambao wataenda kucheza katika klabu kubwa barani Ulaya na kwingineko duniani ili kuwa na timu ya Taifa imara ambayo inaweza kupambana,” amesema Mwangata
SOMA NA HII  YANGA YAITWANGA MTIBWA 1-0