Home Uncategorized OBREY CHIRWA ATOA NENO LA KISHUJAA AZAM FC

OBREY CHIRWA ATOA NENO LA KISHUJAA AZAM FC

OBREY Chirwa, nyota wa Azam FC amesema kuwa ataendelea kutoa burudani ndani ya klabu hiyo baada ya kuongeza kandarasi ya mwaka mmoja.

Nyota huyo jana, Apririli 23 ameongeza dili hilo hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo ya mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho.

“Nipo ndani ya Azam na nitaendelea kuwapa burudani mashabiki wa Azam FC, kikubwa ni kuendelea kutupa sapoti,” amesema.

Ndani ya Azam FC, Chirwa msimu huu ametupia mabao nane na alisepa na mpira mbele ya Alliance FC wakati Azam FC ikishinda mabao 5-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA NA MSAUZI WAPEWA MWAKA MMOJA NA MIEZI SITA