Uncategorized

BEKI HUYU WA UGANDA ATAJWA KUWA KWENYE RADA ZA YANGA

admin April 27, 2020 11:02 am


JUUKO Murshind, beki wa kati anayekipiga ndani ya Klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kurejea Bongo mitaa ya Kariakoo huku Yanga ikitajwa kuwa mstari wa mbele kufuatilia nyendo zake.


Beki huyo ambaye alisepa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa anadai stahiki zake huku mabosi wa Msimbai wakisema kuwa alikuwa ametoroka kambini ilikuwa msimu wa 2018/19.

Habari zinaeleza kuwa Yanga inamhitaji Juuko raia wa Uganda arejee Bongo kumpa nguvu Lamine Moro ambaye amekuwa ni mhimili ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael.

“Kwa sasa uongozi upo kwenye hesabu za kuipata saini ya Juuko hivyo mambo yakiwa sawa anaweza kuibukia Jangwani msimu ujao,” ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mambo mazuri hayahitaji haraka wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi.
WACHEZAJI KUWEKWA HOTELINI KWA MUDA WA WIKI SITA KABLA YA LIGI KUREJEA MTUPIAJI NAMBA MOJA MBAO KUSEPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply