Uncategorized

KOCHA SIMBA: NGUMU KUWAFUATILIA WACHEZAJI KWA SASA

admin April 27, 2020 12:32 pm


SELEMAN Matola, Kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa ni ngumu kwa sasa kufuatilia maendeleo ya wachezaji iwapo wanafanya mazoezi au la wakiwa nyumbani.

Baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na Serikali Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona wachezaji wapo nyumbani baada ya kambi kuvunjwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa hakuna anayeweza kuwafuatilia wachezaji wa Bongo kutokana na mazingira yaliyopo.

“Ni ngumu kuwafuatilia wachezaji wakiwa nyumbani kutokana na mazingira yaliyopo hasa kwetu sisi kibongobongo tunaelewa namna mambo yalivyo.

“Lakini haina maana kwamba kwa kuwa hakuna namna ya kuwafuatilia basi wasifanye mazoezi haitakuwa sawa, mazoezi wafanye na tahadhari wachukue” amesema.

NGOMA BADO NGOMA NZITO AZAM FC KAGERA SUGAR WAO WANAWAFUATILIA KWA MTINDO HUU WACHEZAJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply