Uncategorized

KAGERA SUGAR WAO WANAWAFUATILIA KWA MTINDO HUU WACHEZAJI

admin April 27, 2020 2:02 pm


KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wamekuwa wakiwafuatilia wachezaji wao kwa wakati huu ikiwa wanafanya mazoezi kupitia mitandao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa baada ya ligi kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona walitoa program kwa wachezaji itakayowasaidia kulinda vipaji vyao.

“Tuliwapa program ambayo ni muhimu kwao kuifanya kwa wakati huu wakiwa nyumbani na hiyo itasaidia wao waweze kuwa bora pale ligi itakaporejea.

“Ukweli suala la mazingira kwetu linatuathiri ila ni lazima tuwafuatilie ili kujua wanafanyaje ambapo tumekuwa tukitumia mitandao kufuatilia maendeleo yao kwa namna ambavyo wanafanya mazoezi,” amesema.

KOCHA SIMBA: NGUMU KUWAFUATILIA WACHEZAJI KWA SASA MWANA FA:NIMEPONA CORONA, WADUDU WALINING’ANG’ANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply