Uncategorized

TSHISHIMBI ATOA SHARTI YANGA..!!

admin April 28, 2020 5:13 pm

KIUNGO wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kama kuna kitu anatamani basi ni timu yake kusajili kiungo mpya wa kushindana naye, mwenye ubora hata wa kumzidi.

Yanga katika hesabu zao za usajili wanajipanga kusajili kiungo wa kati mkabaji na kufikia sasa hesabu zinamtaja Mnyarwanda Ally Niyonzima kuwa chaguo la kocha Luc Eymael.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Tshishimbi amesema endapo Yanga itasajili kiungo mkabaji basi itakuwa akili nzuri itakayoboresha timu yao.

Amesema ana kiu kubwa ya kupambana kwa kushindana kwa ubora na kiungo mwenzake aliye na ubora mkubwa ndani ya kikosi hicho.

“Mi napenda sana ushindani, nashangaa watu wanaogopa, mimi niko tofauti sana, napenda ushindani hii ndio njia sahihi ya mafanikio,” alisema Tshishimbi.

“Kukiwa na ushindani mkubwa kwenye timu hapo ndipo ubora wa kikosi unakuja. Yanga wakileta kiungo mkabaji hiyo ndio safi mimi nataka sana tena aje haraka tuwanie nafasi kikosini.”

NDEMLA NA SIMBA KIMEELEWEKA..AWEKEWA FUNGU LA MILIONI 30 KUSALIA MSIMBAZI KIPA YANGA AKODI KOCHA KENYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply