Uncategorized

MSHAMBULIAJI WA YANGA APANIA KUFANYA MAKUBWA, KIWANGO CHAKE ADAI HAKIJAMFURAHISHA

admin April 30, 2020 12:11 pm


DITRAM Nchimbi, shambuliaji wa Yanga amesema kuwa kiwango alichokionyesha kwenye mechi za hivi karibuni akiwa ndani ya klabu hiyo kabla ya ligi kusimamishwa hajakifurahia jambo linalomfanya aongeze juhudi kwenye mazoezi.


Nchimbi alijiunga na Yanga kwenye dirisha dogo akitokea Klabu ya Polisi Tanzania alikokuwa akikipiga kwa mkopo alikuwa ni mali ya Azam FC.

Nchimbi amesema:-“Nilikuwa kwenye ubora ndani ya Yanga lakini sio ule ambao nilikuwa ninauhitaji hivyo kwa wakati huu wa mapumziko ya lazima kutokana na Virusi vya Corona ninafanya mazoezi ili kuwa bora.

“Kikubwa kingine ninachokifanya ni kuomba dua hili janga liishe kwani sio kitu chepesi, ninaamini likiisha na mazoezi ambayo ninafanya nitakuwa kwenye ubora,” .

Nchimbi anashikilia rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick ambapo aliwatungua mabosi wake wa sasa Yanga alipokuwa Polisi Tanzania uwanja wa Uhuru kwenye sare ya kufungana mabao 3-3.
KUHUSU KUPAMBANA NA CORONA WACHEZAJI FANYENI HIVI CORONA KIPIMO CHA UKOMAVU WA WACHEZAJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply