Home Uncategorized KAGERE ANA BALAA KINOMA UWANJANI, MABAO YAKE NI ZAIDI YA 40

KAGERE ANA BALAA KINOMA UWANJANI, MABAO YAKE NI ZAIDI YA 40



MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba amesema kuwa kikubwa kinachomfanya awe bora ni juhudi na kumuomba Mungu jambo.


Kagere amefunga jumla ya mabao 42 ndani ya Ligi Kuu Bara tangu ajiunge na mabingwa hao watetezi msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Gor Mahia ya Kenya.


Msimu wake wa kwanza Kagere alitupia mabao 23 na kuwa kinara kwa wafungaji na Simba ilimaliza ligi ikiwa imefunga mabao 77.

 Msimu huu ligi ikiwa imesimama ametupia mabao 19 akiwa ni kinara pia wa kutupia ndani ya Bongo na kufanya na  Simba imefunga jumla ya mabao 63.

SOMA NA HII  AZAM FC YAKUTANA NA RUNGU LA TFF, MILIONI MOJA YAMEGUKA