HABARI ZA SIMBA-AHMED ALLY
Habari za Simba Leo

MCHANGO WA SIMBA TIMU YA TAIFA UMESHUKA

Abubakar August 26, 2024 12:11 pm

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco ametaja kikosi kitakachojiandaa na mechi za kufuzu Afcon.

Katika orodha ya majina Klabu ya Yanga imetoa wachezaji saba,,Azam wachezaji watano na Simba imetoa wachezaji watatu tu.

Takwimu hizi zinathibitisha kuwa kwa miaka ya karibuni Klabu ya Simba imepunguza mchango wake kwenye kikosi cha Taifa Stars tofauti na miaka mitano iliyopita ambapo ilishuhudiwa mnyama akitoa wachezaji kuanzia sita na kuendelea.

Enzi za ubora wake Simba ndio Klabu iliyokua ikisifika kwa kuwa na wachezaji bora wazawa nchini wakiwemo Aishi Manula,Shomari Kapombe,John Bocco,Erasto Nyoni,Jonas Mkude,Mzamiru Yassin,Kennedy Juma ambao wote hawa hawapo kwa sasa ingawa uwakilishi uliotukuka unasalia kwa Mohamed Hussein Zimbwe Jr aliyepo hadi sasa.

Orodha ya majina .
YANGA
Aboutwali Mshery
Dickson Job
Ibrahim Bacca
Bakari Nondo
Mudathir Yahya
Nickson Kibabage
Clement Mzize
AZAM
Feisal Salum
Adolf Mtasingwa
Pascal Msindo
Nathaniel Chilambo
Lusajo Mwaikenda
SIMBA
Ally Salim
Edwin Balua
Zimbwe Jr

Nyakati zinasogea!ndio maana kwa sasa Simba inapambana kusajili wachezaji vijana wa ndani wakiwemo Valentino Mashaka,Kelvin Kijiri nk ili kurejesha utawala wao!

AHOUA AANZA KAZI SIMBA…MTAFURAHI NA SHOW SLOTI YA STICKY 777 USHINDI X1000 YA DAU LAKO | CHEZA KASINO UWE TAJIRI…