Home Habari za michezo TAIFA STARS YAITAKA AFCON 2025…YAPANGWA NA WAZOEFU…RATIBA IKO HIVI

TAIFA STARS YAITAKA AFCON 2025…YAPANGWA NA WAZOEFU…RATIBA IKO HIVI

Habari za Michezo leo

Taifa Stars imepangwa kundi H katika mashindano ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.

Katika droo ya upangaji makundi ya kuwania kufuzu Afcon 2025, Taifa Stars kwenye kundi lake hilo la H imepangwa pamoja na timu za DR Congo, Guinea na Ethiopia.

Kwa mujibu wa Kanuni za mashindano hayo, timu mbili ambazo zitafanikiwa kuongoza msimamo wa kundi hilo pale hatua ya makundi itakapofikia tamati, zitafuzu kwa fainali za Afcon na mbili za mwisho zitatazama fainali hizo kupitia luninga.

Kalenda iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) inaonyesha kwamba mechi za hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Afcon 2025 zitaanza Septemba 2 na zitafikia tamati Novemba 19 mwaka huu, hivyo Taifa Stars itakuwa na siku 78 za kuhakikisha inapata tiketi ya Afcon mbele ya Guinea, Ethiopia na DR Congo.

Ratiba ya mtego

Taifa Stars itaanzia nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kukabiliana na Ethiopia na baada ya hapo itakwenda ugenini kucheza na Guinea katika raundi ya pili ya mashindano hayo ya kufuzu.

Mechi ya tatu itakwenda ugenini kukabiliana na DR Congo na kisha ndani ya siku zisizozidi saba, timu hizo zitarudiana hapa Dar es Salaam.

Ikimalizana na DR Congo, itasafiri kwenda Ethiopia kuumana na timu ya taifa ya nchi hiyo katika mechi ya raundi ya tano na itamaliza mashindano hayo ya kuwania kufuzu kwa kupambana na Guinea hapa nyumbani.

Mechi za raundi ya kwanza na ya pili zitachezwa kuanzia Septemba 2 hadi 10, zikifuatiwa na zile za raundi ya tatu na nne ambazo zitafanyika kati ya Oktoba 7 hadi 15 na raundi mbili za kufunga dimba zitachezwa kati ya Novemba 11 na 19 mwaka huu.

Kimsingi kwa mujibu wa kalenda hiyo, raundi mbili zitakuwa zikichezwa ndani ya muda usiozidi siku nane (8) jambo ambalo litazifanya timu kuwa na muda mfupi wa maandalizi na mapumziko kutoka mechi moja hadi nyingine.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUENGULIWA SIMBA...KABURU AVUNJA UKIMYA...AGUSIA ISHU YA CHAMA...