Uncategorized

YANGA YAPANIA KUFANYA USAJILI MKUBWA MWAKA HUU, HAWA HAPA HUENDA WAKATUA

admin May 5, 2020 11:29 am


UONGOZI wa wana familia ya Yanga ambao umekuwa ukiipa sapoti timu hiyo katika masuala ya usajili kampuni ya GSM umesema kuwa una mpango wa kuleta mchezaji mkubwa msimu ujao ambae atasaini dili jipya kuitumikia Klabu ya Yanga mwaka huu.

Miongoni mwa usajili ambao GSM imefanya ndani ya Yanga ni pamoja na ule wa Bernard Morrison, kiungo mshambuliaji raia wa Ghana.

Mhandisi, Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Uendeshaji GSM, amesema kuwa wapo vizuri na mpango wao ni kuona wanaleta mchezaji makini atakayekuja kucheza ndani ya Yanga.


 “Mwaka huu kutakuwa na tofauti kubwa ya mwaka jana na tutakuja na mpango tofauti kabisa kuhakikisha kwamba jezi ziuzike ikiwemo ya kuleta wachezaji wapya. 

“Tumejipanga kufanya usajili mzuri na ni ahadi yetu kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga kwamba kuna usajili mkubwa utafanyika mwaka huu,” amesema.

Miongoni mwa nyota wanaotajwa kuwidwa na Yanga ni pamoja na kiungo Ally Niyonzima anayekipiga timu ya Taifa ya Rwanda na Yidah Sven.

MPANGO WA KUREJESHA LIGI,TFF KUNA UMUHIMU WA KUWA NA MKAKATI WA KIPEKEE KULINDA AFYA ZA WACHEZAJI LIVERPOOL INA NAFASI YA KUTWAA TAJI LA ENGLAND, KUNA MPANGO WA KUPUNGUZA DAKIKA 90

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply