NICOLAS Wadada beki chagu
o la kwanza ndani ya kikosi cha Azam FC amewasamehe wapangaji wake kodi kutokana na kupitia wakati mgumu wa kupambana na janga la Virusi vya Corona.
Wadada ambaye ni raia wa Uganda amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na agizo la Serikali ambayo imewaomba wamiliki kufanya hivyo.
Taarifa iliyotolewa Kwenye Ukurasa rasmi wa Instagram wa Azam imeeleza kuwa beki huyo ameamua kuwasamehe kodi wapangaji wake.
“Nina nyumba ambayo niliwapangisha wapangaji na ilikuwa inaniingizia kipato ila kutokana na agizo la Serikali kutaka tuwasamehe kodi wapangaji kutokana na janga la Virusi vya Corona nami nimefanya hivyo,” .