Uncategorized

FIFA YAIBONYEZEA CHEKUNDU TUZO YA MCHEZAJI BORA 2020 MAZIMA

admin May 15, 2020 1:11 pm

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufuta tuzo za soka zinazotolewa na Shirikisho hilo mwaka huu kutokana na janga la Virusi vya Corona. 
Tuzo hizo zilitarajiwa kutolewa jijini Milan nchini Italia, Septemba 2020.

Washindani wawili duniani ambao ni Lionel Messi anayekipiga Barcelona na Cristiano Ronaldo ambao ni washindani wakubwa hawatakuwa na cha kubeba mwaka huu Kwenye kipengele cha Mchezaji Bora wa Mwaka.

Gianni Infantino, Rais wa Fifa amekuwa akiweka wazi msimamo wake kuwa wanachukua tahadhari kubwa dhidi ya janga la Virusi vya Corona. 

Kuhusu tuzo za Ballon d’Or ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu 1956 haijulikani hatma yake mpaka sasa.

MABEKI HAWA WAWILI WA SIMBA PASI ZAO ZA MWISHO ZILIMDONDOKEA KAGERE ISHU YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI ILIYOTINGA TAKUKURU, MEJIBIWA NAMNA HII NA TFF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply