Home Uncategorized DONALD NGOMA NI NGOMA NZITO NDANI YA AZAM FC

DONALD NGOMA NI NGOMA NZITO NDANI YA AZAM FC


DONALD Ngoma, mshambuliaji wa Azam FC ngoma ni nzito ndani ya kikosi hicho msimu huu kutokana na kushindwa kufurukuta kikosi cha kwanza huku akipotezwa na mshambuliaji wa Lipuli, mzawa Paul Nonga kwa kucheka na nyavu.

Msimu uliopita Ngoma alitupia mabao 10 akiwa ni kinara wa kucheka na nyavu huku Nonga wa Lipuli akitupia mabao matano msimu uliopita ila mambo yamebadilika ghafla kwa Ngoma ambaye mkataba wake unameguka msimu huu.

Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 54 ikiwa imetupia mabao 37 Ngoma ametupia mabao mawili tu akipotezwa na Nonga ambaye ametupia mabao 11 kati ya 35 timu yake ikiwa nafasi ya 13.

Bado hatma ya nyota huyo wa zamani ya Yanga kubaki kikosini humo bado ni nzito kutokana na kushindwa kufiti jumla kikosi cha kwanza msimu huu.  

Zaka Zakazi,  Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa masuala ya mikataba kwa wachezaji waliobaki ndani ya Azam FC ripoti ya benchi la ufundi wataamua nani abaki na nani aondoke.

SOMA NA HII  YANGA YAPANIA KUIFANYA SIKU YA WANANCHI YA KIPEKEE ZAIDI