Home Uncategorized MITAMBO MIWILI YA KAZI YANGA NI BALAA, JEZI ZAO WOTE NAMBA SARE

MITAMBO MIWILI YA KAZI YANGA NI BALAA, JEZI ZAO WOTE NAMBA SARE

HERITIER Makambo nyota wa zamani wa Yanga anayekipiga ndani ya Klabu ya Horoya FC anatajwa kurejea ndani ya Klabu hiyo msimu ujao.

Makambo alidumu Yanga msimu wa 2018/19 ambapo alifunga mabao 17 na kuwa ni kinara wa utupiaji jezi yake mgongoni ni namba 19 alipokuwa Yanga.

Pia inaelezwa kuwa Yanga inampigia hesabu pia mshambuliaji Muchael Sarpong ambaye yupo huru kwa sasa naye jezi yake ni namba 19 mgongoni. 

Sarpong alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda alipigwa chini kwa kile kilichoelezwa kuwa aliwaongoza wenzake kufanya mgomo kudai stahiki zao za mwezi Machi.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mipango ya usajili ipo wakati ukifika ila sio sasa kwa kuwa wakati bado.

SOMA NA HII  YANGA WAPEWA KIUNGO WA MABAO,HUKO SIMBA WAANZA KUTANDA,NDANI YA SPOTIXTRA JUMAPILI