Uncategorized

MTUPIAJI NAMBA MOJA AKUBALI KUTUA YANGA MAZIMA

admin May 18, 2020 10:28 am

PAUL Nonga, mtupiaji namba moja ndani ya Klabu ya Lipuli amesema kuwa yupo tayari kusaini ndani ya Yanga iwapo ofa yao itakuwa inaeleweka kwani yeye ni mwanajeshi hachagui kambi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa aliwahi kucheza Yanga zama za Hans Pluijm na aliamua kuondoka bila ugomvi hivyo hana tatizo na Yanga.
“Niliwahi kucheza ndani ya Yanga zama zile za Pluijm ila niliamua kuondoka kwa kuwa wakati ule sikua chaguo la kwanza kwa sasa tayari nimeshawaaga mabosi zangu Lipuli kuwa nitaondoka na ninaweza kucheza Yanga iwapo ofa yao itaeleweka kwangu.
“Wakati ule na sasa mambo yamebadilika haina maana kwamba nitakosa nafasi hapana uwezo wangu umekuwa na kila siku ninazidi kuwa bora, ninasubiri na kuona ofa yao itakuaje kwani ninazo ofa nyingi,” alisema.
Nonga ndani ya Lipuli amehusika kwenye mabao 15 kati ya mabao 35 ambapo amefunga 11 na ametoa pasi nne za mabao.
YANGA YAZIDIWA UJANJA KWA SIMBA YAPISHANA NA KIUNGO HUYU FUNDI WALIYEKUWA WAKIMPIGIA HESABU SIMBA WAVUNJA REKODI ZILIZOWEKWA NA AZAM FC PAMOJA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply