Uncategorized

SIMBA WAVUNJA REKODI ZILIZOWEKWA NA AZAM FC PAMOJA NA YANGA

admin May 18, 2020 10:28 am

MABINGWA watetezi Simba msimu huu wa 2019/20 kabla hata Ligi Kuu Bara kuisha wamevunja rekodi mbili za mabingwa wa zamani ambao ni Yanga na Azam FC.
Azam FC ambao ni washindani wakubwa wa Simba na Yanga imetwaa taji la ligi mara moja ilikuwa ni msimu wa 2013/14 na ilitwaa taji hilo baada ya kufikisha pointi 62 kibindoni.
Yanga, mabingwa wa kihistoria wa taji la ligi ambapo kabatini wana mataji 27 msimu wa 2014/15 walitwaa taji hilo wakiwa na pointi 55 kibindoni.
Pointi hizo zote zimevunjwa na Simba ambapo kwa sasa ni vinara wa ligi baada ya kucheza mechi 28 kibindoni wana pointi 71 na wamebakiwa na mechi 10 kumaliza mzunguko wa pili ila kwa sasa ligi imesimama kutokana na janga la Virusi vya Corona.
MTUPIAJI NAMBA MOJA AKUBALI KUTUA YANGA MAZIMA CORONA YAIVURUGAVURUGA KABISA MBAO FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply