Home Uncategorized MERTENS AINGIA ANGA ZA CHELSEA

MERTENS AINGIA ANGA ZA CHELSEA


DRIES Mertens, aliyeletwa duniani Mei 6,1987 kwa sasa ana umri wa miaka 33 anatajwa kuingia rada za Chelsea.

Mshambuliaji huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya Napoli akiwa anatumia jezi namba 14 inaelezwa kuwa mabosi wa Chelsea wameelewa uwezo wake.

Alitua Napoli msimu wa 2013 akitokea Klabu ya PSV ambapo huko kwa msimu wa 2011/13 akiwa PSV amecheza mechi 62 na kufunga mabao 37.

2013 mpaka maimu huu wa 2019/20 ndani ya Napoli amecheza mechi 226 na kufunga mabao 90.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA WAJIVIKA MABOMU KUMALIZANA NA POWER DYNAMO