Uncategorized

MIRAJI ATHUMANI ATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI WAKE

admin May 21, 2020 7:17 am

MIRAJI Athuman ‘Sheva’ ambaye anashikilia rekodi ya kuwa ‘super sub’ wa Simba msimu huu akiwa ameshikilia mabao ya Meddie Kagere amesema kuwa yupo fiti.

Sheva kabla ya kuumia misuli ya nyama ya enka mwaka jana alipokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania alionyesha maajabu kwenye ligi, akifunga mabao sita huku pasi yake moja na penalti mbili alizosababisha mbele ya Mbeya City na Kagera Sugar zikifungwa na Kagere mwenye mabao 19.
Maajabu yote haya Sheva aliyafanya ndani ya dakika 508 alizocheza akiwa amehusika moja kwa moja kwenye mabao tisa ya Simba kati ya 63, akiwa na wastani wa kuwa na hatari langoni kila baada ya dakika 56.

Sheva amesema kuwa anamshukuru Mungu ametenda maajabu kwani ameanza kurejea kwenye ubora wake.
“Ukweli napenda kumshukuru Mungu kwa kuwa nimeshaanza kurudi kwenye ubora wangu, naamini ligi ikianza nitakuwa moto,” amesema Sheva.

Mechi alizocheza ni tisa kati ya 28 ambazo ilikuwa namna hii:-JKT Tanzania (30), Mtibwa Sugar (27) Kagera Sugar (29), Biashara United (83), Azam FC (33), Singida United (81), Mwadui (45), Mbeya City (90), Ruvu Shooting (90).

Chanzo: Championi
ULIMWENGU: NITACHEZA NDANI YA YANGA HAYA HAPA MABAO YA BERNARD MORRISON WA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply