Uncategorized

JEMBE JINGINE LA KAZI LINALOTUA SIMBA NI NOMA

admin May 26, 2020 9:47 am

MEDDIE Kagere mshambuliaji namba moja ndani ya Simba jina lake linatajwa pia kuwa miongoni mwa nyota ambao watarejea mapema kuungana na wachezaji waliobaki Bongo kuanza mazoezi.

Kagere aliibukia Rwanda baada ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na Janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.

Habari zinaeleza kuwa tayari jitihada zimeanza kufanyika kumrejesha nyota huyo ili aendelee pale alipoishia kwenye ligi akiwa ni kinara wa utupiaji.

“Kagere ni miongoni mwa nyota ambao wanaweza kurejea mapema kwani uongozi unatambua mchango wake hiyo ataungana na wachezaji wenzake mapema,” ilieleza taarifa hiyo.

Kagere ndani ya ligi ni kinara wa kutupia mabao ambapo amefunga mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao huku Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao 63.

IDRISA SULTAN BADO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWENYEKITI BIASHARA UNITED: TULIKUWA NA HALI MBAYA SANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply