Uncategorized

MWENYEKITI BIASHARA UNITED: TULIKUWA NA HALI MBAYA SANA

admin May 26, 2020 10:47 am


SELEMAN Mataso, Mwenyekiti wa Klabu ya Biashara United ameshukuru kupokea msaada wa mipira 19 kutoka kwa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Msaada huo ni kwa ajili ya kuipa sapoti timu hiyo kwenye maandalizi ya kukamilisha mechi tisa zilizobaki.

 Mataso amesema, “Tulikuwa na hali mbaya sana katika suala la mipira hivyo huu msaada utatusaidia kwa kiasi kikubwa sana katika mazoezi yetu,”.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Musoma Benedict Magiri amesema michezo ni sehemu ya sera ya chama hicho hivyo msaada huo ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya chama hicho.

Tayari kikosi cha Biashara United Mara leo kimeanza mazoezi rasmi kipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 29 ikiwa na pointi 40.

JEMBE JINGINE LA KAZI LINALOTUA SIMBA NI NOMA KUMEKUCHA JANGWANI, YAMALIZANA NA JEMBE HILI LA KINYARWANDA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply