Uncategorized

MWENYEKITI WA ZAMANI WA SIMBA RAGE HAJAFANYA MAAMUZI KUHUSU KUGOMBEA TENA UBUNGE

admin May 26, 2020 8:47 am


MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Rage amesema kuwa hajaamua mpaka sasa kama atagombea ubunge ama hatagombea kwa kuwa anapima upepo ajue mambo yatakuaje.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa kudaiwa kuwa alikuwa ameanza kufanya kampeni za siri jambo ambalo ni kinyume na katiba.

Rage ambaye ni mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, aliwekwa mahabusu kuanzia Mei 23 hadi Mei 24 ambapo aliachiwa kwa dhamana.

Rage amesema:-“Nikawauliza iweje tangu tangu tarehe 16 mje kunihoji leo siku 73 zimepita? Kwanza mimi sijatangaza nia mpaka sasa wala sijaamua kwamba nitagombea au sitagombea. Napima upepo kwanza. Mimi kwetu Tabora na bahati mbaya mbunge ambaye yupo sasa hatokei Tabora sasa nahisi labda ana hofu na mimi.”

MESSI: TUNATAKIWA KUBADILI AINA YA UCHEZAJI ILI TUSHINDE MAMBO BADO HAYAJAWA SHWARI NDANI YA ENGLAND

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply