BAHATI Vivier, Kocha Msaidizi wa Azam FC, amewasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zake 54.
Azam FC imeanza kufanya mazoezi yake jana Jumatano ikiwa ni maandalizi ya kumalizia mechi zake 10 zilizobaki baada ya kucheza mechi 28.
Vivier atakuwa akifanya kazi na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar,wakisubiria kurejea nchini kwa Kocha Mkuu, Aristica Cioaba na Kocha wa Viungo, Costel Birsan, waliokwama nchini kwao, Romania.
Makocha hao wanasubiria kurejea kwa usafiri wa ndege katika anga la Ulaya mwezi ujao, kufuatia makampuni mengi ya usafiri wa anga kusimamisha shughuli zao baada ya mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Corona (COVID-19).