Home Uncategorized KAHATA MAMBO BADO NCHINI KENYA

KAHATA MAMBO BADO NCHINI KENYA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa bado ni ngumu kwa kiungo wao wa Kenya Francis Kahata kuibuka Bongo kwa sasa kutokana na mipaka ya huko kufungwa kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa bado wanaendelea kufanya mawasiliano na wachezaji ambao hawajawasili ili kujua namna gani wanaweza kujiunga na wachezaji wengine.

“Bado kuna ugumu kwa nyota wetu ambao wapo nje ikiwa ni pamoja na Kahata kwani ni suala la mipaka kufungwa na Serikali hivyo pale mipaka itakapofunguliwa itakuwa rahisi  kutua.

“Tunafanya mawasiliano na wachezaji wetu wote ili kujua namna gani wanaweza kurejea nchini kuendelea na maandalizi ya mechi zetu ambazo zipo mbele yetu,” amesema.

Jana wachezaji wa Simba waliwasili kambini na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wao wa Bunju kwa ajili ya maandalizi ya mechi za za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.

Kahata amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akihusika kwenye mabao 10 ya Simba kati ya 63 akipachika kimiani manne na kutoa pasi sita za mabao.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU