Home Uncategorized HIVI NDIVYO WACHEZAJI YANGA WALIVYOMKOSESHA MKWASA LAKI MBILI NA TISINI

HIVI NDIVYO WACHEZAJI YANGA WALIVYOMKOSESHA MKWASA LAKI MBILI NA TISINI


MASTAA 29 wa Klabu ya Yanga ambao wameanza mazoezi hivi Mei 27 katika chuo cha Sheria walimnyima Kocha Msaidizi, Charlse Mkwasa kiasi cha sh.290,000,(laki mbili na elfu tisini)

Yanga imeanza mazoezi ya pamoja Mei 27 kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe za Shirikisho.

Picha lipo namna hii, kabla ya kuanza mazoezi hivi karibuni, Mkwasa aliwaambia wachezaji wake kuwa yeyote atakayeangusha mojawapo ya vikwazo (Cone) atakatwa 10,000.

Jambo hilo liliwafanya wachezaji kupambana kufanya vema na licha ya kufanya zoezi hilo zaidi ya mara moja hakuna aliyedondosha kikwazo hicho.

Kwa hesabu hizo, wachezaji 29 walipambania sh.10,000 zao hivyo Mkwasa kushindwa kuambulia chochote.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI TANZANIA BARA