Uncategorized

HESABU ZA SIMBA KUSEPA NA UBINGWA ZIMEKAA NAMNA HII

admin June 2, 2020 9:47 pm


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni kuona anaiongoza timu hiyo kusepa na taji la Ligi Kuu Bara kwa kushinda mechi zake tano za mwanzo.


Ikiwa Simba itasepa na ushindi kwenye mechi tano itavuna pointi 15 na kufikisha pointi 86 ambazo haziwezi kufikia na timu yoyote ndani ya ligi kwa sasa ina pointi 71.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13 kufuatia Serikali kuruhusu masuala ya michezo kuanza kuanzia Juni Mosi.

Sven amesema:-“Mipango ya timu ni kuhakikisha tunapata pointi 15 katika michezo yetu mitano ya mwanzo ili kutwaa ubingwa wa Ligi mapema.”


Hakukuwa na mechi ya ushindani tangu Machi 17 kutokana na Serikali kusimamisha masuala ya michezo kwa sababu ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Mchezo wa Simba, Juni 14 utakuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Taifa.

HIVI HAPA VIGONGO 11 VYA YANGA NDANI YA LIGI KUU BARA, RATIBA YAKE SIMBA YAIPIGA BAO YANGA KWA BEKI KISIKI, NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply