KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa hana tatizo na kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu ana imani atafanya naye kazi kwa ukaribu.
Hivi karibuni, Sven alimchimbisha kambini Ajibu kwa kueleza kuwa alichelewa kambini bila kutoa taarifa wakati Simba iliporiti kambini Mei 27.
“Sina tatizo na Ajibu ila ukiwa ni kiongozi lazima usimamie nidhamu ili kuweka usawa kwa wachezaji wengine wakati mwingine lakini kama ni tatizo sina tatizo na Ajibu atabaki kuwa mchezaji wa Simba.
“Tunahitaji kuona kila mchezaji anakuwa na nidhamu makini ambayo ni silaha ya kufika kule ambako tunaelekea na kikubwa ni kufuata utaratibu ambao upo siku zote,” amesema.
Kwa sasa Ajibu yupo kambini na wachezaji wenzake ambao wanajiweka sawa kwa ajili ya mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.
Mchezo wa Juni 14, Simba itamenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa.
KOCHA AFUNGUKA KUHUSU NAFASI YA AJIBU SIMBA
SOMA NA HII SIMBA KUKOSA HUDUMA YA NYOTA WAKE WAWILI JUMLA, WENGINE WAWILI WATEGEMEA MAAMUZI YA SVEN