Uncategorized

LUSAJO NYOTA WA KMC ALIYEIBUKIA KUTOKA NAMUNGO ATAJA MABAO ATAKAYOFUNGA

admin November 2, 2020 6:47 am


 MSHAMBULIAJI wa KMC, Relliants Lusajo, ameweka wazi kuwa mikakati yake msimu huu ni kuifungia timu hiyo mabao yasiyopungua 15 katika Ligi Kuu Bara, huku akiamini yataisaidia timu hiyo kufanya vizuri.

 

Lusajo amejiunga na KMC msimu huu akitokea Namungo ambapo msimu uliopita alimaliza ligi akifunga mabao 13, huku msimu huu akiwa na KMC amefunga mabao matatu katika michezo mitano aliyoichezea timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Lusajo alisema: “Malengo yangu ni kufunga mabao mengi iwezekanavyo, sitaki kuweka malengo niwe mfungaji bora ila nahitaji nifunge mabao mengi yasiyopungua 15 ambayo naamini yataisaidia timu yangu katika kujiweka kwenye nafasi nzuri.

 

“Msimu huu utakuwa na ushindani wa mabao kwa watu wengi kwa kuwa kuna ongezeko la washambuliaji wengi bora ambao licha ya kuwa bado hawajafunga, lakini naamini huko mbele watafunga sana na kuleta ushindani.”

 

Lusajo mbali na kuwa tegemeo kwenye Ligi Kuu Bara, pia anatazamiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya KMC kwenye mchezo ujao dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Karume. 


BERNARD MORRISON NA SHOMARI LAWI WANATUACHIA MASWALI MAGUMU POGBA: NILIFANYA KOSA LA KIJINGA NDANI YA UWANJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply