Uncategorized

KESHO NI YANGA V KMC UHURU

admin June 6, 2020 1:47 pm


KESHO Yanga itakuwa na kibarua kingine cha kumenyana na KMC kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja na Azam TV na unatarajiwa kuwa wa kukata na shoka kwa kuwa Yanga ina kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi hivyo kwao inaweza kuwa sehemu ya kulipa machungu.

Majira ya saa 10 jioni utapigwa mchezo huo huku kiingilio kikiwa ni buku tano VIP  na buku tatu kwa mzunguko.

Huo utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Yanga wa kirafiki baada ya masuala ya michezo kuruhusiwa na Serikali, walianza na Transint Camp na kushinda kwa mabao 3-1 kisha Dar City wakashinda mabao 2-0 kesho zamu ya KMC.

KIPA KMC NA SIMBA KIMEELEWEKA….KOCHA KMC AANIKA KILA KITU AZAM FC YAPANDISHA MAJEMBE SITA YA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply