Home Uncategorized KMC: SIO BONGO TU, HATA ULAYA TIMU HUWA ZINATETEREKA

KMC: SIO BONGO TU, HATA ULAYA TIMU HUWA ZINATETEREKA


JUMA Kaseja,nahodha wa Klabu ya KMC amesema kuwa walitetereka mwanzoni mwa mzunguko wa kwanza jambo lililowafanya watafute mbinu ya kurejea kwenye ubora wao.

Kaseja amesema kuwa mambo hayo ya kutetereka siyo Bongo tu hata Ulaya inatokea kwenye maisha ya soka.

“Siyo Bongo tu hata Ulaya yapo masuala ya kuyumba mwanzoni mwa msimu ila mwisho wa siku mambo huwa yanakaa sawa ndivyo ilivyokuwa kwetu pia.

“Bado tuna mechi mkononi ambazo ni tisa katika hizo tutapambana kupata matokeo mazuri hilo linawezekana,” amesema.

KMC imecheza mechi mbili ngumu za kirafiki kujiandaa na kuendelea na mechi za ligi, ambapo ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Yanga na ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 na Simba.

Ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza jumla ya mechi 29 kibindoni ina pointi 33. 

SOMA NA HII  SIMBA YAZIDI KUJIBU MAPIGO JANGWANI, KAHATA, SHAMTE NI MUDA WOWOTE, YUPO MMOJA YANGA