KOCHA mkuu wa Mbao FC, Abdulmutik Hajji amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi zao zote zilizobaki ili kujinusuru kushuka daraja msimu ujao.
Hajji amesema kuwa mbinu pekee itakayowabakisha wao ndani ya ligi ni kushinda mechi zake zilizobaki kwa kupambana kupata matokeo chanya.
“Tuna kazi ngumu ya kucheza mechi tisa ambazo zimebaki nazo ni ngumu, tunatakiwa kushinda ili kubaki kwenye ligi msimu ujao kwani hatupo kwenye nafasi nzuri,” amesema.
Mbao ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 huku ikisalia na michezo 9.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.