Uncategorized

MBEYA CITY YAGOMA KUSHUKA DARAJA

admin June 9, 2020 4:47 pm

AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mapambano ya ligi kwa mechi ambazo zimebaki.

Mbeya City imebakiwa na mechi tisa ili kukamilisha mzunguko wa pili wa ligi huku wakiwa kwenye hatari ya kushuka daraja iwapo watashindwa kuchanga karata zao vizuri.

Said amesema:”Tunatambua tunachokitaka ndani ya ligi, mechi zetu ambazo zimebaki tutapambana kupata matokeo chanya ili tubaki kwenye ligi msimu ujao kwani wachezaji wapo tayari na morali ni kubwa,” amesema.

Ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni imejikusanyia pointi 30 ikiwa nafasi ya 17.

YANGA WAMALIZANA NA STRAIKA ,MBELGIJI SIMBA AMKOMALIA CHAMA, KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO SIMBA YATUA KWA MUUAJI WAO NA YANGA,GSM YAANZA NA MASTAA HAWA,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply